Update:

Umoja wa Ulaya wapongeza serikali ya Burundi kwa kuwaacha huru wafungwa 740


Umoja wa Ulaya wapongeza serikali ya Burundi kwa kuwaacha huru wafungwa 740 waliokuwa wamekamatwa katika katika matukio ya mwaka 2015

Umoja wa Ulaya wapongeza serikali ya Burundi kwa kuwaacha huru wafungwa wapatao 740 waliokuwa wamekamatwa tangu mwaka 2015  kufuatia ghasia na vurugu zilizosababishwa na maandamano na jaribio la mapinduzi.

Ujumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi amepongeza uamuzi wa wizara ya sheria nchini Burundi kwa kuwaacha huru wafungwa 740 waliokuwa wamekamtwa katika matukio tofauti waliofuatia jaribio la mapinduzi. Miongoni mwa watu walio achiwa huru, 450 walihusika na matukio ya mwaka 2015.
Taarifa hiyo ilitolewa katika tovuti ya Umoja wa Ulaya na kuomba vijana wachwe huru vijana wote waliokamatwa katika maandamano ya mwaka 2015.