Update:

Ujerumani yamkosoa Trump juu ya hatari ya vita vya kibiashara na EU

Msemaji wa Serikali ya Ujerumani ameikosoa Marekani juu ya uwezekano wa kutokea vita vya kibiashara kufuatia hatua ya Washington kuongeza kiwango cha ushuru wa forodha kwa bidhaa za Ulaya.

Steffen Seibert amesema kuwa, maamuzi ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuzijumuisha bidhaa za Ulaya katika ushuru mpya wa forodha ni njia isiyo sahihi ambayo inaweza kuzusha vita vya kibiashara. Msemaji wa serikali ya Ujerumani amefafanua kwamba, kutokea vita vya kibiashara kutakuwa na madhara kwa watumiaji wa pande zote mbili.Steffen Seibert,

Alkhamisi iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa, sera za uingizaji bidhaa ya aluminiumu ni pigo kwa sekta ya uzalishaji wa ndani nchini Marekani na hivyo aliamua kupandisha ushuru wa furodha kwa bidhaa feleji na asilimia 10 kwa aluminiamu za mataifa ya Ulaya zinazoingizwa nchini humo. Baada ya hapo Umoja wa Ulaya ulitishia kuchukua hatua kali mkabala wa hatua hizo za Washington, huku Trump pia naye akitoa vitisho dhidi ya nchi hizo za Ulaya iwapo zitachukua hatua yoyote dhidi ya nchi yake.David Lidington, Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May

Wakati huo huo siku ya Jumatatu David Lidington, Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, alikosoa vikali vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani vya kuanzisha vita vya kibiashara na Umoja wa Ulaya. Lidington, ambaye pia ni mjumbe wa ngazi ya juu wa baraza la mawaziri nchini Uingereza alisema kuwa, maamuzi ya Marekani juu ya kuanzisha vita vya kibiashara na Umoja wa Ulaya sio ya busara na hayatokuwa na maslahi kwa upande wowote ule.