Update:

Tanzania yashinda 2-0 dhidi ya DRC, Uganda yatoka sare 0-0 na Sao Tome, Kenya yafungwa 3 - 2na Afrika ya KatiJijini Dar es Salaam, Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi wa magoli 2-0 ilipocheza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (The Leopards), katika mechi ya kirafiki iliyochini ya mwamvuli wa FIFA.


Magoli ya Tanzania dhidi ya timu hiyo inayoshika nafasi ya tatu kwa viwango vya ubora wa soka Afrika yalifungwa na Mbwana Samatta pamoja na Ramadhani Kichuya, na kuifanya timu hiyo sasa ivune pointi tatu katika mechi mbili kwa kuwa katika mechi ya kwanza walipoteza dhidi Algeria wiki iliyopita.

Kwa upande wao (The Cranes) timu ya taifa ya Uganda, wakiwa katika uwanja wa Namboole mjini Kampala wamejikuta wakilazimishwa sare ya bila kufungana na Malawi (The Flames).

Kocha wa Uganda Sebastien Desabre amesema mechi hiyo ni sehemu ya michezo ya maandalizi kwa ajili ya kuzikabili Tanzania na Lesotho mwezi Septemba kwenye mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2019.

Hii ilikuwa mechi ya pili kwa Uganda katika siku nne ambapo katika mechi ya kwanza waliibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Visiwa vya Sao Tome and Principe.

Habari haikuwa njema jijini Nairobi, baada ya wenyeji Kenya (Harambee Stars) kukubali kipigo cha magoli 2-3 walipocheza dhidi ya timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Magoli ya Kenya yalifungwa na Eric Omondi katika dakika ya 17, na jingine likiwa ni la kuchelewa katika dakika ya 90 lililofungwa na Michael Olunga

No comments