Update:

TAARIFA MAALUMU KWA WATEJA WA AUWSA

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira jiji la Arusha  (AUWSA)  Inawatangazia wateja waliositishwa huduma ya maji kuwa mamlaka inawapa fursa ya kulipa madeni au kufika ofisi za mamlaka ya maji na kuingia makubaliano ya malipo ya deni kwa awamu na kurudishiwa huduma ya maji safi

Usiate adha ya kukosa huduma ya maji kwani utaratibu wa kulipa deni lako kwa awamu umewekwa na AUWSA kwa manufaa yako   Njoo sasa uingie makubaliano na AUWSA ,Tumia fursa hii ni ya mudu 

Pia mamlaka inawaarifu wadaiwa wote kuwa zoezi la kusitisha huduma kwa wadaiwa linaendelea ,Lipa deni lako kwa wakati kuepuka usumbufu 

Kwa maelezo na maelekezo zaidi wasiliana na AUWSA huduma kwa wateja kwa namba 0800110069
(bure) au wafikie ofisi na. 22 AUSA kwa msaada zaidi 


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA ARUSHA