Update:

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUMO MPYA WA MALIPO YA LUKU


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wote wanao tumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, 2018 TANESCO itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa Taasisi za Serikali.

TANESCO ikiwa miongoni mwa Taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, Kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki.

Serikali kwa kushirikiana na Wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike kwamba, TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa Taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio, baadhi ya Taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji.

TANESCO inapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka.

TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA:OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

No comments