Update:

Shilingi million 400 zatolewa kwaajili ya Ukarabati wa Zahanati ya Nkaiti

Serikali imetenga kiasi cha shilingi million 400 kwaajili ya Ukarabati wa Zahanati ya Nkaiti ili kuipandisha hadhi kuwa kituo cha Afya.
na kutatua kero ya ukosefu wa huduma za  afya katika  kata ya Nkaiti  iliyopelekea   wagonjwa wengi kupoteza maisha wakati wakizifuata huduma hizo Mkoa wa Arusha,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Hamisi Malinga alisema zahanati hiyo ya Nkaiti ilikuwa ikihudumia Vijiji vyote Vitano pamoja na Makambi ya Watalii yaliyoko jirani na hifadhi ya Tarangire.
Alisema Uboreshwaji wa kituo hicho cha Afya utasaidia kuhudumia wananchi zaidi ya Elfu ishirini na tatu wa vijiji vyote vya kata hiyo na kuwahudumia watalii wanaopita kwenye Ushoroba wa Tarangire Manyara na wale walio na hoteli za kitalii Manyara na Tarangire.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Olasiti Daudi Mollel alisema wameupokea mradi huo kwa furaha kwani awali mgojwa anapougua walimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Mponduli au Arusha hivyo kupata mradi huo ni jambo la kipekee kwao.