Update:

Papii Kocha: Kukosea ni sehemu ya kujifunza

 Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na redio Clouds leo Machi 9,2018, Papii Kocha amesema kuwaachia huru wafungwa kutawapa nafasi ya kujifunza upya maisha ya uraiani.

"Kuna watu wamefungwa tangu miaka ya 1980 na tumewaacha jela. Mtu akikaa kule anatakiwa kuja kuungana na jamii ili tuone kama amebadilika," amesema.

Papii Kocha na baba yake Nguza Viking maarufu kwa jinala “Babu Seya”ambaye pia amehojiwa katika kipindi hicho, ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Aidha, amesema kuachiwa kwao huru kutoka katika kifungo cha maisha ilikuwa kama bahati kwao kwa sababu hawakufikiria kama wangetoka. "Tulivyofungwa tulidhani tutaachiwa.Tulikata rufaa ya kwanza mwaka 2005 ikadunda, ya pili ilikuwa 2010 lakini pia haikufanikiwa. Tuliamua kumuachia Mungu," amesema.