Update:

Pambano la Machi 31 Uingereza; Bondia Anthony Joshua amuonya mpinzani wakeBingwa wa uzito wa juu katika mchezo wa Ngumi Anthony Joshua AJ wa Uingereza amemuonya Joseph Parker wa New Zealanand ambaye ni mpinzani wake katika pambano litakalofanyika machi 31 mjini Cardiff.

Katika maneno yake, AJ amemwambia Joseph ajiandae na pambano gumu ambalo litaamua bingwa wa mkanda wa WBO.

Katika hatua nyingine AJ amekubali uwezo mkubwa wa kupigana alionao Joseph.