Update:

"Nimeambiwa nimeathirika tangu mwaka 2002 na hadi leo naishi" – Mr. Nice



Mwanamuziki Mr. Nice amefunguka na kujibu tetesi zinazodai kuwa ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Tuheshimiane’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa tetesi hizo zimekuwepo kwa kipindi kirefu hivyo ni kitu ambacho hakimshangazi.

“Nimeambiwa Mr. Nice ameathirika tangia mwaka 2002 na mpaka leo naishi, halafu hapo katikati tushazika wengi sana, so what about me,” amesema.

“Mashabiki zangu wale huwa hawaumizi kichwa, wanasemaga tunamjua Mr. Nice. Maadui zangu wapo tu hawajifichagi, wamemtafuta Nice kwenye kuvuta bangi hawampati, kwenye skendo za wanawake hawampati,” ameongeza Mr. Nice.

Katika hatua nyingine Mr. Nice amezungumzia hatua ya hasimu wake kimuziki, Dudu Baya kuacha pombe. Mr. Nice amesema jambo hilo si la kumpongeza kwani Dudu Baya anaweza kuwa ameshuka kiuchumia akaamua kuchukua hatua hiyo.