Update:

Ngorongoro heroes kushuka dimbani kukipiga na Morocco TaifaTimu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Morocco ,mchezo utakaochezwa Machi 17, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya DR Congo utakaochezswa Machi 31, 2018.

Morocco wanatarajia kutua Tanzania Machi 14,2018 ikiwa na msafara wa watu 31 wanaojumuisha wachezaji 23 na viongozi 8 wa benchi la ufundi.

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni.