Update:

NEY WA MITEGO APEWA ONYO NA NAIBU WAZIRINAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza amemtaka Msanii Emmanueli Elibariki maarufu Ney Wamitego kuacha kutumia maneno yenye utata yanayolenga kuleta mmomonyoko wa maadili ya mtanzania anapoandaa nyimbo zake.

Shonza ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam ambapo japo Serikali inafahamu sanaa ni ajira, lakini ajira hii imekua ikitumika vibaya kwa kuharibu maadili ya mtanzania kulingana na maneno yanayotumika sambamba na kuwa na mavazi ya uchi katika picha jongevu hivyo kudhalilisha utu hasa kwa mwanawake.

Amesema Ney wa Mitego wamemuonya kutokana na nyimbo anazozitoa kutumia maneno yenye utata.

Pia wakati mwingine kuwa na picha jongevu zinazodhalilisha utu wa mtu na kwam a walikubaliana naye atabadilika na kuzingatia maadili ya mtanzania kwa kazi zake za mbeleni.

Wakati huohuo Shonza ameigiza BASATA kuanzia sasa inapotokea kuwa wimbo unatolewa na msanii yeyote na unakiua maadili ya mtanzania wimbo huo uchukuliwe hatua kwa haraka.

Wakati huohuo Ofisa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) Rolf Kibaja amesema rai kwa vituo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia kanuni za utangazaji.

Amefafanu vituo hivyo vinapopewa leseni hupewa na sheria na kanuni za uendeshaji wa vituo hivyo.

“Hivo tunawataka waandaaji na wasimamizi wa vipindi kuzingatia kanuni hizo kwani Mamlaka ya mawasiliano imejipanga kuhakikisha kuwa nyimbo zote zitakazokua zinaenda kinyume na maadili zitachukulia hatua kwa mujibu wa sheria kanunu na taratibu zilizopo,” amesema Shonza.

Akizungumza baada ya kauli ya Shonza Ney Wamitego ameishukuru wizara hiyo kumweka sawa na kumpa nafasi nyingine ya kujirekebisha katika kazi zake za sanaa.

Ney wa Mitego ameahidi kufanya mambo mazuri yatakayokuwa tofauti na aliyowahi kufanya awali.

Amesema lengo la wizara ni kuona anafanya kazi ambazo zipo kwenye ubora unaokubalika na kwamba atatumia kipaji chake kwenye muziki huo kuwa na kazi ambazo zitazingatia sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa.