Update:

Mwili wa mwanafunzi Mtanzania aliyeuawa Afrika Kusini wiki mbili zilizopita unazikwa leo huko Kigoma.

Baraka Nafari aliyekuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Mwanza aliuawa usiku wa kuamkia Februari 23, huko Johannesburg, Afrika Kusini na watu wasiofahamika. Habari zinasema aligongwa na gari mara mbili kwa kubamizwa ukutani.
Nafari alikuwa nchini humo akichukua masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg na alitarajiwa kuhitimu Juni mwaka huu.
Binamu wa marehemu, Uwezo Edward, anayeishi Cape Town alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema utata wa mazingira ya mauaji yametokana na ushahidi wa video ya (CCTV) wa siku ya tukio katika eneo alipokuwa ndugu yake huyo.