Update:

Mmiliki wa klabu ya ligi kuu afungiwa kutoingia uwanjani kwa miaka mitatu kwa kosa la kuingia na silaha uwanjani

Rais wa klabu ya PAOK Salonika inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ugiriki Ivan Savvidis amepewa adhabu ya kutoingia kwenye viwanja vya mpira kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na kosa la kuingia uwanjani na bastola.


Machi 11, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni hasira baada ya mwamuzi kukataa goli la timu yake kwenye mechi dhidi ya AEK Athens, Saviddis aliingia uwanjani pamoja na mashabiki wengine jambo lililozusha vurugu kubwa na kupelekea serikali kusimamisha ligi kwa muda.

Kutokana na tukio hilo, timu yake ilipokwa pointi 3, imepigwa faini ya Yuro 63,000 na adhabu ya kucheza mechi tatu za ligi bila mashabiki, na Savvidis mwenyewe akipigwa faini ya Yuro 100,000.

Ligi ya Ugiriki inatarajiwa kurejea mwishoni mwa juma hili baada ya Chama cha soka cha nchi hiyo kujadiliana na Serikali juu ya usalama viwanjani.