Update:

Messi aanza mazoezi na Argentina kwa ajili ya mechi dhidi ya Italia itakayopigwa ijumaa hiiLionel Messi jana ameungana na wachezaji wenzake katika timu ya taifa ya Argentina inayojiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Italia kwa ajili ya kujipima ubavu kuelekea mashindano ya kombe la dunia.

Messi amefika jana na kujiunga na timu iliyoko kambini katika uwanja wa Manchester City na rasmi akaanza mazoezi ili kukipa nguvu kikosi cha timu hiyo ambacho kitamkosa mashambuliaji Sergio Aguero aliyemajeruhi.

Mechi ya Argentina na Italia itapigwa usiku wa ijumaa katika uwanja wa Etihad mjini Manchester.