Update:

Matokeo ya mechi 8 za hatua ya 16 bora za UEFA Europa League zilizochezwa usiku wa jana


Hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League ilichezwa usiku wa machi 8 kwa michezo nane ya kwanza kuchezwa barani Ulaya. Hatimaye Arsenal yang'ara na kuitandika AC Milan 2-0, huku Dortmund ikikubali kulala kwa 2-1 dhidi ya Salzburg, CSKA Moskva ikikubali kipigo cha 1-0 toka kwa Lyon, na Atletico Madrid ikiifunga Lakomotiv Moskva 3-0, Sporting Cp wao wameifunga Plzen 2-0, nayo Marseille ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Athletic Club, RB Leipzig yenyewe imeshinda 2-1 ndihi ya Zenit, na Lazio imetoka sare ya 2-2 na Dynamo Kyiv.