Update:

Mapishi ya nyama na pilipili boga na pilipili hohoMahitaji: Nyama ya ng'ombe,pilipili boga,  pilipili hoho, vitunguu saumu , mchuzi wa sosi vijiko viwili, wanga kijiko kimoja, sosi ya chaza vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja.

Njia:

1.kata nyama ya ng'ombe iwe vipande, changanya pamoja na wanga, mchuzi wa sosi na mafuta. Kata pilipili boga na pilipili hoho ziwe vipande?

2.washa moto, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga, halafu tia vipande vya vitunguu saumu, pilipili hoho na pilipili boga, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi na sosi ya chaza, chembechembe za kukoleza ladha na chumvi, korogakoroga,ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

No comments