Update:

Mamia wajitokeza Ngorongoro MarathoniWanariadha 1,000 wanatarajiwa kutimua vumbi katika mashindano ya riadha Ngorongoro yaliyopangwa kufanyika Aprili 21, 2018.

Mashindano hayo yanashirikisha wanariadha wa ndani na nje ya Tanzania, yatafanyika kwa mara ya 11 tangu kuanzishwa mwaka 2008.

Mratibu wa mashindano hayo Petro Meta amesema mashindano ya mwaka huu yatashirikisha wanariadha zaidi ya 500 na yamegawanyika katika makundi matatu yam bio a kilomita 21, kilomita 5 na kilomita mbili na nusu.