Update:

MAMA KANUMBA AMWAGA MACHOZI STENDI KUONA BANGO LA KANUMBA THE GREAT

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba 'Kanumba the Great' ameshangaza wengi baada ya kuanza kumwaga machozi katika moja ya stand zinazojaza watu jijini Dar es salaam baada ya kuona bango lenye picha ya mtoto wake katika maeneo hayo.

Mama huyo ambae alishindwa kuzuia hasira zake na kulia alisema kuwa mara nyingi amekuwa akiumia sana na kushindwa kujizuia kutoa machozi kila anapoona picha au kitu chochote ambacho kinamkumbusha mtoto wake.

"Kila mara nimekuwa nikiziona picha za kanumba katika mabango , lakini sijui kwanini hii imenifanya nipatwe na uchungu na niishiwe na nguvu kabisa.-Alisema Mama Kanumba ambae anasema kuwa alikuwa akielekea maeneo ya segerea kwa ajili ya kurekodi movie.

Kanumba alifariki miaka zaidi ya mitano iliyopita baada ya kuuawa na mpenzi wake (Lulu Michae) waliokuwa na mtafaruku na kusababisha mauaji yake pindi walipokuwa wakizozana.

Hata hivyo Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baaada ya kukuta na hatia ya kuua bila kukusudia.