Update:

LHRC yadai upinzani ulionewa uchaguzi mdogo Kinondoni na Siha.....Hapa Kuna Tamko Lao

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.

Akizungumza jana Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," alisema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana.”


==>Soma Tamko lao hapo chini