Update:

Kocha wa Al Masry achekelea sare ugenini


Kocha wa Al Masry Hossam Hassan amefurahia matokeo ya sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Simba huku timu yake ikiwa ugenini ikicheza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Hossam ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Zamalek mwaka 2003 kilichovuliwa uningwa wa Afrika na Simba amesema mechi ilikuwa ngumu lakini anafurahia matokeo waliyopata ugenini ambayo anaamini yatakuwa msaada kwenye mechi yao ya nyumbani.“Tumefunga magoli mawili, haya ni matokeo mazuri kwetu hapa Tanzania japo sio kwa asilimia 100 lakini hii ni mechi ya kwanza, tutakuwa na mechi ya pili nyumbani tunawaheshimu wapinzani wetu (Simba) wanakocha mzuri.”

“Dakika 15 za mwisho zilikuwa ngumu kwa sababu uwanja ulikuwa na maji ukizingatia nilikuwa natumia wachezaji wengi vijana.”“Mchezo wa marudiano natarajia utakuwa mgumu kwa sababu tukirudi nyumbani tutacheza mechi moja ya ligi kabla ya kukutana na Simba lakini tutakuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo.”