Update:

Kocha Mkuu wa Gicumbi FC ajiuzulu wadhifa wake kufuatia matokeo mabaya


Kocha wa klabu ya Gicumbi FC inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda Godfroid Okoko ametangaza kujiuzulu wadhifa akiwa bado ndani ya mkataba na klabu hiyo ambayo inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo.


Okoko amedai kuchukua uamuzi huo kufuataia matokeo mabaya ya timu yake kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi msimu huu.

Akisisitiza uamuzi wake huo aliochukua baada ya mechi dhidi ya APR ambayo timu yake ilifungwa magoli 4-0 ikiwa nyumbani, amesema ni vyema akatoa nafasi kwa wengine wajaribu kuisaidia timu kutoshuka daraja.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Methode Kamali amepewa jukumu la kuiongoza timu hiyo hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

Habari zilizoenea nchini Rwanda ni kwamba kocha Okoko tayari ameanza mazungungumzo ya kujiunga na klabu nyingine ya ligi hiyo Espoir FC