Update:

Fc Basel wanaweza kukamilisha ratiba kwa kipigo kikubwa pale Etihad hii leo

Ukiniuliza mimi ni nini kitawatokea Basel hii leo mbele ya City nitakuambia sijui, lakini pia ninajua kwamba Fc Basel japo mpira unadunda lakini kwa sasa ni ngumu sana kuwagusa hawa City wa Pep Gurdiola(Wako On Fire).
Kwa rekodi tu za Champions League hakuna timu ambayo ilifungwa bao 4 kwa nunge katika hatua kama hii halafu wakaja kufanikiwa kupindua mabao hayo na kufudhu kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Cha kutisha zaidi kuhusu Basel ni kwamba Man City hakuna timu ambayo imewahi kuwafunga katika mechi zao 12 za mwisho Etihad katika Champions League huku michezo yao minne ya mwisho wakishinda yote.
Hiyo michezl 12 ya mwisho pia, City hawajawahi kuacha kufunga. Yaani ina maana katika mechi hizo 12 za mwisho za Man City kikosi hicho kilifanikiwa kupata bao katika kila mchezo.
Pep Gurdiola anataka kuifikia rekodi ya Carlo Ancelotti na Bob Paisley ya kuchukua michuabo ya Champions League mara tatu kwani hadi sasa amechukua mara mbili na zote akiwa na klabu ya Barcelona(2009 & 2011).