Update:

Fahamu Tabia za Wanawake Wanaopenda Sana Pesa
1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima.
Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao.

Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya.

Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako.

Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa.

2. Wengi hutoka familia masikini.
Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi.

Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini.

Umasikini wako usikufanye ujidharau au mtu akudharau. Lipo kundi dogo la wanawake wanaojitahidi kutetea thamani ya jinsia yao lakini wengi wao ni wakuonewa huruma tuu.

3. Wengi wao hawana elimu ya kutosha.
Mwanamke aliesoma akaelimika hawezi hangaika na pesa ya mtu. Ndio maana wanawake wachache huhangaika kwajili ya kujitegemea na sio kumtegemea mwanaume.

Wanawake wengi wenye elimu na vipato vizuri huwezi msikie akiongelea pesa Kama kigezo muhimu kwa mwanaume anayemuhitaji awe mume wake.

4. Ni wavivu na wasio na mawazo.
Wanawake wote wanaopenda pesa ni wavivu kupita kiasi. Uvivu wao umeanzia akilini kiasi kwamba hawana mawazo ya maendelo. Utakuta mwanamke anawaza mambo mepesi kabisa Kama urembo, nguo, mtoko, n.k.

Wanawake wapenda pesa ni hatari kwa ustawi wa familia.
Huwezi kuwa na familia kubwa ukiingia katika bahari ya viumbe hawa.

5. Hawana shukrani wala uvumilivu.
Wanawake wapenda pesa huwezi msikia akikushukuru zaidi ya kujichekesha tuu na kubinua makalio.

Kwa mfano amekuomba milioni moja then ukampa laki tano basi utamsikia akisema sasa hii nitafanyia nini, au niongezee tena mume wangu huku akikushika kifua au ndevu.

Wanawake wenye hekima hushukuru mpaka mwanaume anasikia aibu.

Suala la uvumilivu halipo kwa hawa wanawake. Shida ikitokea ukishindwa kuitatua kwa wakati huo basi hesabu umeliwa. Yaani kwao kukusaliti ni jambo lisilo na mashaka.