Update:

Droo kwa ajili ya mechi za robo fainali Klabu Bingwa Ulaya kufanyika kesho ijumaa mjini Nyon nchini Uswisi.



Droo kwa ajili ya kupanga mechi za robo fainali za klabu bingwa Ulaya inatarajiwa kufanyika kesho ijumaa katika makao makuu ya UEFA mjini Nyon nchini Uswisi majira ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Timu nane zitakazopambanishwa katika droo hiyo ni Barcelona (Hispania), Bayern M√ľnchen (Ujerumani), Juventus (Italia), Liverpool (Uingereza), Manchester City (Uingereza)

Real Madrid (Hispania), Roma (Italia) na Sevilla (Hispania).

Mechi za robo fainali zinatarajiwa kupigwa tarehe 3 na 4 mwezi Aprili, ikiwa ni mechi za awali, na marudiano tarehe 10 na 11 mwezi Aprili.