Update:

Diamond kushiriki wimbo maalum Kombe la Dunia 2018


Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz anatarajiwa kushiriki katika wimbo maalumu wa Kombe la Dunia. Wimbo huo utakuwa unawakilisha bara la Afrika.

Wimbo huo ambao umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.

Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka March 16 mwaka huu.

Leo Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June mwaka huu.