Update:

Diamond atangaza kufunga ndoa, aomba baraka za mama yake

Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz ametumia siku ya leo ya Wanawake Duniani kumtakia kheri mama yake mzazi na kutangaza mipango yake ya ndoa.

Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu ametumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram kufikisha ujumbe huo kwa mama yake huku akiweka wazi mpiango yake ya kuvuta jiko mwaka huu.
Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini…..Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka….. @mama_dangote
Mnamo Febuari 14, mwakahuu mzazi mwenzake na Diamond Zarina Hassani alitangaza kuachana na mkali huyo wa ‘Waka Waka’ kwa madai ya kutokuwa mwaminifu katika mahusiano yao.