Update:

CHIMBUKO LA WAIRAQ!


WAIRAQ au Wairaki ni kabila kubwa
linalozungumza lugha jamii ya Wakushi na
linalopatikana Mkoa wa Manyara wilaya za
Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha
katika wilaya ya Karatu.
Watu wa kabila hilo wanauhusiano wa asili na
makabila ya Gorowa, Burungi na Alawa ambao
wanaishi katika wilaya za Babati na Kondoa.
Historia kwa njia ya simulizi za makabila inasema
chimbuko la Wairaqw linatokana na kizazi cha
watu wa kale walivyokuwa wakiishi eneo la
Mesopotamia, Iraq.
Vita ya mara kwa mara ilisababisha watu hao
kuhama makazi yao ya asili katika karne ya nne
hadi ya sita baada ya kuzaliwa kwa Kristo.
Wairaqw walivuka bahari ya Sham kwa mashua
na kutua Ethiopia ambako waliishi kwa muda
kisha kuendelea kuhama kuelekea Kusini
Magharibi kupitia bonde la ufa kando ya Ziwa
Victoria na kuweka kambi eneo waliloona ni
salama.
Kwa kuwa ni watu wasiopenda vita waliendelea
kuhamahama wakikimbia vita vilivyoruka sehemu
mbalimbali walizojaribu kuweka kambi. Walipita
njia ya kati kupitia Iramba Mkoa wa Singida
Iramba hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa
ambapo walikutana na mapambano ya Wahehe,
Wangoni na Wazimba.
Hali hiyo iliwalazimu kubadilisha njia na kurejea
kuelekea Kaskazini hadi sehemu ya Kondoa
mahali panapoitwa Guser Tuwalay na kuishi eneo
hilo huku wakijishughulisha na ufugaji na kilimo
kidogo. Hata hivyo ilitokea kutokuelewana kati
yao na watu wa kabila la Wabarbaig jambo
lililosababisha vita.
Ingawa walikuwa waoga wa vita walikuwa na
silaha za kujihami dhidi ya vita. Walitumia mikuki
na mishale ya asili ilitengenezwa na miti
iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma
unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye
ncha kali na baadaye waligundua zana
zinazotengenezwa kwa kutumia udongo wa
mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali
kama tofali.
Hata hivyo Wairaq walishindwa vita na kukimbilia
karibu na mlima Hanang kisha wakagawanyika
wengine wakaelekea mlima Dabil hadi Guser na
Gangaru ambapo walifanya maskani. Wairaq
walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo,