Update:

Babu apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kulawiti wanafunzi wa shule ya msingi NamangaMkazi mmoja wa kijiji cha Buguruni kata ya namanga wilaya ya longido mkoani arusha Babu Abdurahaman msuya maarufu kwa jina la “babu wa mafuta taa” mwenyewe umri wa miaka arobaini na mbili amepandishwa mahakamani wilayani Longido kwa makosa ya ubakaji na ulawiti.

Katika mashtaka hayo, mtuhumiwa anatajwa kuwa na kesi tofauti ikiwa ni pamoja na Kesi namba 186 inamkabili kusiana na suala la ulawiti kwa watoto ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi namanga ,shule ya awali namanga pamoja na shule ya AIC namanga

Kesi hiyo ya namba 186 yenye makosa matatu inayohusisha wanafunzi wa kike wawili pamoja na wa kiume mmoja imesemekana tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 6 Novemba mwaka 2017.

Kesi zote hizi zinazoendesha na mwendesha mashtaka wa mahakama ya wilaya ya longido Anzelimu Mhella chini ya hakimu mkazi mwandamizi Mfawidhi wilayani hapa Aziza Emily Temu alisema upelelezi umekamilika na kesi inaendelea kusikilizwa na kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe (21/03/2018).