Update:

AZAM KUJIPIMA NGUVU KWA FRANCE RANGERS KABLA YA KUVAANA NA MTIBWA SUGAR


 

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wanawakaribisha France Rangers katika dimba lao la nyumbani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

France Rangers ni timu ambayo imemaliza msimu huu daraja la kwanza Mkoa wa Dar es Salaam yenye kikosi kizuri na wachezaji walio fiti uwanjani.

Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya timu hizo mbili utachezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi utakaofanyika kesho Jumamosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari Azam FC Jaffary amesema pamoja na kikosi chao kinaendelea na mazoezi kukabiliana na Mtibwa sugar katika mchezo wa robo Fainali kombe la FA machi 31 mwaka huu, mwalimu na benchi la ufundi kuweza kuwapima wachezaji kwa kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya France Rangers ya Dar es Salaam.

"Ni sehemu tu ya benchi la ufundi na mwalimu kuweza kuangalia baada ya mazoezi ya wiki moja na nusu pengine tu ni kutaka kuona kiwango cha wachezaji pamoja na uwezo wa kila mchezaji walichokielewa katika hazoezi hayo" amesema Jaffary.

Amesema katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao mahiri wanne ambao ni Himidi Mau, Yahaya Zayd na Shabani Chilunda ambao wameitwa katika timu ya Taifa (Taifa Satars),mwengine ni Daniel Amor kutoka Ghana ambaye ni majeruhi.

"Mchezaji wetu nyota wa kimataifa kutoka nchini Ghana Daniel Amor anasumbuliwa na tatizo la goti, uongozi utamsafirisha Amor Siku ya Jumatatu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu" amesema Jaffary.