Update:

ASKARI ATAKAYE KAMATA MADEREVA WANAOWASHAWISHI KUPOKEA RUSHWA WATAANDISHWA VYEO
Jeshi la polisi mkoani Pwani limeanzisha kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva wanao washawishi askari kupokea rushwa pindi wanapokutwa na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani Jonathan Shana amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema Jeshi hilo litawapandisha vyeo askari watakao wakamata madereva wanaojaribu kuwashawishi wapokee rushwa.

Aidha, Kamanda Shana amesema watafanya ukaguzi wa magari ya mizigo yanayobeba abiria hususani yale yaendayo kwenye magulio mbalimbali, pia magari aina ya noah yanayozidisha abiria pamoja na yale yanayobeba wanafunzi bila ya kuwa na ubora.