Update:

Ally Hapi awataka walio vunja nyumba ya Msanii wa bongo fleva Mandojo kujisalimisha kabla hawajaanza kutafutwa

Tangu Jumatano kumekuwa na picha na video zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mandojo akilalamika kuvunjiwa nyumba yake na watu wasiojulikana wakati yeye akiwa safarini.
 


Sasa taarifa nzuri ni kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amezipata taarifa hizo na tayari ameshawasiliana na Man Dojo na leo Machi 31, 2018 ameahidi kwenda Mbweni kuangalia uharibifu uliofanyika kwenye nyumba hiyo.
Hapi amewataka watu hao waliovunja nyumba hiyo kujisalimisha mara moja kabla ya hatua za kuwatafuta hazijaanza.


Mchana huu nimeona clip ya msanii Man Dojo ikimuonesha akilalamika kuvunjiwa nyumba yake aliyoijenga kwa jasho lake la muziki na watu asiowajua akiwa safarini. Watu hao (mabaunsa) wanatajwa kufanya tukio hilo kata ya Mbweni wilayani Kinondoni ngawa video haielezi ni mtaa gani.Ofisi yangu haina taarifa yoyote ya kuvunjwa nyumba eneo la Mbweni. 
Yeyote mwenye kumfahamu Man Dojo naomba amjulisha kuwa aje anione nyumbani kwangu kesho jumamosi saa 2 asubuhi.Na hao waliofanya tukio hilo popote walipo,wajisalimishe kabla sijawatafuta!,“amesema Ally Hapi kwenye taarifa yake.


Kwa mujibu wa maelezo ya Man Dojo amesema kuwa watu hao hawajulikani kuwa walitoka wapi kwani hata serikali ya mtaa haikuwa na taarifa na watu hao na kwa sasa Man Dojo na familia yake wanalala nje baada ya tukio hilo.


No comments