Update:

Afrika Mashariki ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na majanga duniani mwaka 2017Ukame eneo la Afrika Mashariki na mafuriko makubwa wakati wa pepo za monsuni katika Bara Hindi ni baadhi ya mambo yaliyosababisha mwaka 2017 kuwa mwaka uliogubikwa na matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa WMO limesema hayo Ijumaa katika ripoti yake iliyotolewa kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Hali ya Hewa, maudhui yakiwa kujiandaa kukabili hali ya hewa na kutumia maji kwa ufanisi.

Ripoti inasema matukio ya hali ya hewa kwa mwaka 2017 yameathiri maendeleo ya kiuchumi, uhakika wa chakula, masuala ya kiafya na pia uhamiaji.

Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema viwango vya joto kwenye eneo la ncha ya kaskazini mwa dunia vilikuwa ni vya juu kuliko kawaida huku maeneo yenye watu wengi ya kaskazini mwa dunia yakigubikwa na baridi kali pamoja na vimbunga vikali vya theluji.Ongezeko la Joto duniani

Ripoti hiyo imesema Kenya na Somalia ziliendelea kukumbwa na ukame huku mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ukikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.

Mwaka uliopita wa 2017 umetajwa kuwa mwaka uliovunja rekodi ya joto kali zaidi katika historia ya sayari ya dunia pasina kuwepo tukio la El NiƱo huku kukiwa na wasi wasi kuwa hali itazidi kuwa mbaya katika miaka ijayo.

Taalas amesisitiza kwamba mwenendo wa muda mrefu wa ongezeko la joto ni jambo linalotia wasiwasi kuhusu mustakbali wa dunia.