Update:

AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI KWENYE MSAFARA WA RAIS MAGUFULI KAHAMA

Mkazi wa Kahama aliyejulikana kwa jina la Deogratius Landani (47) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari mojawapo miongoni mwa magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


Tukio hilo limetokea Jumamosi Machi 10,2018 majira ya saa 7:00 mchana katika mtaa wa Shunu kwenye njia kuu ya kutoka Masumbwe kueleke Kahama wakati magari yakiwa kwenye msafara wa rais Magufuli wilayani Kahama.


Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Kasyombe Mwakyusa Chanzo ni mpanda baiskeli huyo Deogratius Landani kuingilia msafara kwa kuingia barabarani ghafla bila kuchukua tahadhali za kutosha.


Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji Kahama kwa uchunguzi zaidi.


chanzo:Malunde1 blog