Update:

Nyoso afungiwa mechi 5 kwa kosa la kumpiga shabiki

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia mchezaji Juma Nyoso kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Ameadhibiwa kwa kuwa vitendo kama hivyo ni kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia mchezo wa kiungwana.
Kamati imemtia hatiani Juma Nyoso kupitia kanuni za ligi kuu na katiba ya TFF lakini ilipokea taarifa za nyuma za Nyoso kwamba aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kwa hiyo kamati imemfungia Nyoso mechi tano pamoja na faini ya shilingi 1,000,000 (milioni moja).