Update:

Mwanasheria mkuu wa Kenya ajiuzulu

Mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai ametangaza kujiuzulu hii leo baada ya kuhudumia  kwa kipindi cha miaka 6. Kupitia mtandao wa Twitter Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Muigai ambapo amesema amepokea barua hiyo kwa masikitiko na amemshukuru kwa uongozi wake uliotukuka katika kipindi hicho cha miaka 6.
Kufuatia kujiuzulu kwa muigai Rais Kenyatta ametangaza kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa Paul Kihara Kariuki kuwa mwanasheria mkuu wa Taifa hilo.
Pamoja na uteuzi huo Rais Kenyatta amefanya uteuzi mwingine ambapo amemteua Kennedy Ogeto kuwa solisita mkuu katika ofisi ya mwanasheria mkuu, Abdikadir Mohammed kuwa balozi wa Kenya nchini Korea Kusini na Njee Muturi ameteuliwa kuwa Naibu Afisa anaeshughulikia ofisi ya Rais.