Update:

Mahakama kutoa uamuzi maelezo ya onyo ya Halima MdeeMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi Mosi,2018 itatoa uamuzi iwapo maelezo ya onyo yaliyotolewa polisi na mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee yapokewe kama kielelezo au la. Mdee anashtakiwa kwa kutumia lugha ya fedheha kwa Rais John Magufuli.

Awali, shahidi wa upande wa mashtaka D/SSGT Arbogast aliomba kuyatoa maelezo hayo ya onyo mahakamani kama kielelezo lakini wakili wa utetezi, Peter Kibatala alipinga akidai yalichukuliwa nje ya muda.

Hakimu mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kusikiliza pande hizo mbili amesema Machi Mosi,2018 atatoa uamuzi iwapo maelezo hayo ya onyo yapokewe kama kielelezo au la. Mdee anadaiwa Julai 3,2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema iliyopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, alitumia lugha fedheha dhidi ya Rais.