Update:

HIMID MAO KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Baada ya kukosa michezo mitatu mfululizo kutokana na kupata majeraha, nahodha na kiungo wa Azam FC, Himid Mao, huenda akapelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.


Kiungo huyo alikosa mchezo dhidi ya Simba hivi karibuni ambao timu yake ilipoteza kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, alisema kuwa kiungo huyo ana tatizo la goti na amekuwa akitibiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi).


Aidha alisema kutokana na hali hiyo na maendeleo yake baada ya vipimo anatarajiwa kuwasilisha suala hilo kwa uongozi ikiwezekana kwenda kutibiwa Sauz.


“Himid bado kuweza kurejea uwanjani kutokana na tatizo la goti ambalo kwa sasa linamsumbua na anatibiwa katika Taasisi ya Mifupa, Moi na kutokana na jinsi alivyo sasa tunasubiri vipimo kisha nitapeleka kwenye bodi ya timu kuweza kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.

“Kwa sasa hana uwezo wa kurejea uwanjani kutokana na hilo tatizo, pale atakapokuwa fiti na akatibiwa kabisa wakati ukifika hilo tutaweza kuwaeleza pia,” alisema Mwankemwa.