Update:

WAFUASI WA ODINGA WAZUILIWA KWENDA KUSHUHUDIA KUAISHWA KWA KIONGOZI WAONairobi, Kenya. Mabasi matatu yaliyokuwa yakisafirisha wafuasi wa muungano wa upinzani wa Nasa kutoka Mombasa yamezuiwa Voi kwenye kaunti ya Taita Taveta.Mabasi hayo yalikuwa miongoni mwa mabasi sita yaliyoondoka Mombasa kwenda Nairobi yakiwa na wafuasi hao waliokuwa wanakwenda kushuhudia tukio la kuapishwa kwa viongozi wao Raila Odinga na Kalonzo Musyoka.
Mkuu wa polisi wa Voi Joshua Chesire alisema magari hayo yalikamatwa kutokana na “makosa ya usalama barabarani ". Yalikamatwa saa 9:00 alfajiri.
"Kwenye mabasi hayo walikuwemo abiria 82 ambao hawakuwa pia wamezingatia masuala ya usalama. Wengi wao ni vijana ambao 10 hawakuwa na vitambulisho. Miongoni mwao ni wanawake wanne," alisema Chesire.
Aliongeza kwamba abiria hao watafikishwa kortini na watashtakiwa kwa makosa juu ya usalama wa barabarani.
Chesire alisema mabasi hayo yaliruhusiwa saa 2:00 kuendelea na safari yao.
Hata hivyo, madereva wa mabasi hayo waliliambia shirika la Nation kwamba wanarudi Mombasa na waliendesha kuelekea Mombasa.