Update:

Mwigulu amnadi Mollel jimbo la Siha

CHAMA cha mapinduzi ccm jana kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro ambapo Waziri wa mambo ya ndani na M'bunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mh Mwigulu Nchemba alimnadi mgombea wa chama hicho Dr Godwin Mollel.
Awali akifungua kampeni hizo Mwigulu alisema kuwa ccm ni chama kinachotekeleza sera zake kwa wananchi na kutatua kero za watanzania kwa kiasi kikubwa nani chama makini kinacho thamini shida za wananchi na kuwataka wasilubuniwe kwa namna yeyote ile iwe ya kidini kikabila n.k.
"Ewe mwanachi wa Siha na unauchungu wa maendeleo yako Piga kura kuichagua Ccm pasipo kujali kwani maendeleo hayana chama na M'bunge aliyepangwa na Ccm ni Dr Mollel kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Siha" alisema Mwigulu.
Nae kwa upande wake mpeperusha bendera ya chama cha mapinduzi Ccm Dr Godwin Mollel aliwashukuru wananchi walioweza kumlaki na kumuunga mkuno kwa asilimia zaidi ya 85% ya jimbo hilo na kumuhaidi kumpigia kura za ndio na kumrudisha bungeni kwa tiketi ya chama hicho cha mapinduzi kilichopo madarakani ili kuweza kutatua kwa kina changamoto za wananchi hao wa Siha huku migogoro mingi ikiwa ni migogoro ya Ardhi.