Update:

MSAKO DHIDI WATOTO YA WANAOFANYABIASHARA ZISIZO RASM ARUSHA WABAINI ZAIDI YA WATOTO 100

Watoto zaidi ya 100 wameokolewa kutoka kwenye biashara  zisizo rasmi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara mbalimbali ikiwemo kutumwa na wazazi wao na kuweka kando masomo ya shuleni.

Msako huo ambao umeanza soko la Kilombero jijini Arusha umesisimua baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakitafuta njia mbadala ya kutaka kuwasaidia watoto hao lakini hawakuwa na ufumbuzi

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiendesha msako huo, Afisa tarafa ya Themi Felisiani Mtaingelwa amesema lengo la msako huo ni ili kuweza kutekeleza ahadi ya raisi ya elimu bure ili kila mtoto apate haki yake ya msingi kwa kuweza kujiendeleza kimasomo

Kwa upande wake Raphael Mkombe ni afisa tarafa ta Themi amesema kuwa atahakikisha kuwa watoto hao wanarudi mashuleni na kuendelea na masomo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wazazi wao ili waweze kuelezea sababu za watoto hao kuishi mazingira hayo.