Update:

Magunia 328 ya Bangi yenye uzito wa kilo 6703 yateketezwa Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha

Na Michael Nanyaro
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya nchini imekamata na kuteketeza madawa ya kulevya aina ya bangi magunia 328 yenye uzito wa kilo 6703 katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha huku watuhumiwa 18 wakiwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa  madawa hayo.
Akizungumza katika zoezi la uteketezaji wa madawa hayo aina ya bangi kamishna wa sheria wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Edwin Kakolaki amesema kuwa mamlaka hiyo imeendelea kupambana na matumizi ya madawa hayo ambapo katika msako ambao waliufanya katika wilaya hiyo waliweza kukamata bangi hizo katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Aidha pamoja na kuzungumza hayo ametoa onyo kali kwa wasafirishaji wengine wa madawa hayo ya kulevya ambao walikuwa wakitumia bahari ya hindi kama uchochoro wa kupitisha dawa hizo kuacha mara moja biashara hizo kwani mamlaka hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao wameshuhudia uteketezaji wa bangi hizo,wanapongeza hatua hiyo huku wakilitaka jeshi la polisi kuweka kambi zao mashambani ili kumaliza kabisa mizizi hiyo ya ulimaji wa zao hilo.
Katika kipindi cha mwaka 2017 serikali iliongeza nguvu zaidi katika suala la upambanaji na madawa ya kulevya ambapo inaelezwa kuwa kuanzia zoezi hilo lilipoongezewa nguvu utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana umepungua.