Update:

Jose Mourinho kuachana na Manchester United 2020

Kocha Jose Mourinho ameongezewa maktaba wa kuifundisha klabu ya Manchester United Jose Mourinho hadi mwaka 2020 na katika mkataba wake huo mpya pia kukiwa na kipengele cha nyongeza ya mwaka mmoja endapo atafanya vyema.


Mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Bw. Ed Woodward amesema wameamua kumuongeza Mourinho mkataba kutokana na mafanikio aliopata katika msimu wake wa kwanza kitu ambacho hakuna kocha mwingine ambaye amewahi kufanya hivyo.

Upekee wa Mou ni kwamba, aliweza kutwaa kombe la EFL mwezi Februari mwaka jana, pia alitwaa kombe ambalo hakuna kocha mwingine aliwahi kulinyakua katika historia ya klabu ambalo ni kombe la Yuropa jijini Stockholm.
Woodward pia amekiri kuwa tangu Mourinho atue United, amerejesha imani, ameongeza ari na motisha kwa mashabiki na klabu kwa ujumla.