Update:

Barcelona yafuzu nusu fainali

Klabu ya Barcelona imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mfalme nchini Hispania (Copa Del Rey) baada ya kuiondoa Espanyol kufuatia ushindi wa magoli mawili kwa sifuri kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali iliyofanyika jana.

Magoli ya Barcelona katika mechi hiyo yalifungwa na Lionel Messi moja na Luis Suarez moja.
Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Nou Camp, nyota Felipe Coutinho alicheza kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo.
Timu zingine zilizofuzu nusu fainali ya kombe hilo ni, Sevilla, Valencia na Leganes.