Update:

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva anazidi kubeba vichwa vya habari kutokana na kasi na mchango wake anaozidi kuutoa katika klabu yake ya Difaa El Jadid.

Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Morocco, Msuva jana ameipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania Agadir.

Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo.