Update:

Cecafa, Zanzibar na Uganda kucheza nusu fainali leo


Cecafa, Leo ni leo mjini Kisumu ambapo Zanzibar na Uganda wanacheza nusu fainaliKuhusu mechi ya pili ya nusu fainali inayopigwa leo mjini Kisumu, kocha mkuu wa Zanzibar Hemed Suleiman amesema, kwa kutumia vipaji alivyonavyo kwenye kikosi chake watajitahidi kutafuta matokeo mazuri kwenye mechi dhidi ya Uganda, ili kuendeleza rekodi nzuri waliyopata kwenye mashindano ya msimu huu.

Lakini kwa upande wake kocha wa the Cranes, Moses Basena, yeye amekiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi za hatua ya makundi, na kwamba kupitia uzoefu walionao kwenye michuano hiyo watajitahidi kushinda mechi hiyo ili kuingia fainali.

No comments