Update:

Basi la shule lagongana na treni Ufaransa

Basi moja la shule limeripotwa kugongana na treni na kusababisha vifo vya watoto wanne huku wengine 19 wakiwa wamejeruhiwa nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa habari,ajali hiyo imetokea Perpignan jioni ya Alhamisi.
Majeruhi wanasemekana kuwa na hali mbaya.
Kuna uwezekano wa idadi ya vifo kuongezeka.
Basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi kati ya miaka 13-17.

No comments