Update:

ZUIO LA SHAIDI WA 12 SAKATA LA KESI YA MAUWAJI YA BILIONEA MSUYA LA IBUA MVUTANO MKUBWA MAHAKAMANI
Mvutano wa kisheria umeibuka katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi baada ya shahidi wa 12 upande wa mashtaka kuweka mapingamizi mawili likiwamo la kumkataa asitoe ushahidi.

Utata huo uliibuka baada ya shahidi wa 12, Ponsian Severine Cloud kukataliwa na upande wa utetezi kwa madai kuwa jina lake halikuorodheshwa kwenye mashahidi wala halikusomwa katika commital proceeding (kufungasha ushahidi kwenda mahakama kuu).

Cloud anayetoka Mahakama ya Mwanzo Moshi Mjini, aliitwa kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya. Aliieleza mahakama hiyo kuwa yeye ndiye aliyechukua maelezo ya mshtakiwa wa tano, Karim Kihundwa baada ya kufikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia inasikilizwa na Jaji Salma Maghimbi.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne, Musa Mangu, Jalila Zuberi, Kihundwa, Sadik Mohamed na Ally Mussa.