Update:

ZAIDI YA NG’OMBE 10,000 ZA UGANDA NA RWANDA KUPIGWA MNADAWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametangaza kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 10,000 wa nchi za Uganda na Rwanda waliokamatwa katika operesheni inayoendelea nchini.

Mpina alitangaza hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019.

Waziri huyo ambaye alikuwa akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge amesema ng’ombe hao watapigwa mnada wakati wowote kama ilivyofanya kwa ng’ombe 1,325 wa Kenya.

Amesema uhusiano wa Tanzania nchi nyingine washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni mzuri na akisisitiza hakuna ushirikano wa kihalifu. Mpina amesema walioingiza ng’ombe hao ni wahalifu na wamevunja sheria za nchi na kutahadharisha wafugaji wa nchi jirani kufuata sheria wanapotaka kuingiza mifugo nchini.

No comments