Update:

WAZEE WA KIMILA WAMEHASWA KUZILINDA NA KUZITETEA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII YAO ARUSHA

Katika kutokomeza vitendo vya kikatili na ukiukwaji wa haki za mtoto  viongozi na wazee wakimila hasa katika kabila la kimasaai wamehaswa kuzilindaa na kuzitetea haki za mtoto katika jamii yao

Wakizungumza viongozi hao wa rika pamoja na ukoo wa kabila la kimasaai  katika warsha iliyoandaliwa na shirika la SOS  Children Villegge kwaajili ya kuwakutanisha na na maafisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya arusha ili kuwaelimisha ushiriki wao wa kuzilinda na kuzitetea haki za watoto  wazee hao wamesema

Katika jamii yao vitendo hivi vipo kwa mila ambazo walikuwa nazo ila watashirikiana na serikali na jamii kwa ujumla ili utokomeza mila ambazo zinamnyima haki mototo katika jamii yao wameomba wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu
Akizungumza katika warsha hiyo afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya arusha(ARUSHA DC) Josina Mlaki  ameelezea kuwa ukiukwaji wa haki na mtoto ni changamoto kubwa katika halmashauri yao 
Kwa upande wao wadau ambao wameandaa warisha hiyo shirika la SOS Children Village wamezungumzia lengo la kuandaa warsha hiyo
Halmashauri ya Arusha inachangamoto kubwa ya ukiukwaji wa haki za watoto kama ubakwaji ukeketaji wa watoto wa kike ndoa za utototni na nyingine nyingi ambapo kata zinazoongoza kwa vitendo hivyo   Olimotonyi Mwandeti Bwawani Kiranyi Kisongo. 

No comments