Update:

TFDA YAZIFUTIA USAJILI NA KUZUIA MATUMIZI YA DAWA MABALIMBALI ZA BINADAMU ZINAZO LETA MADHARA KWA WAGONJWA
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imezifutia usajili dawa mbalimbali za kutibu magonjwa ya binadamu na kuziondoa kwenye soko pamoja na kusitisha matumizi yake kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa wagonjwa.

Hayo yameelezwa Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya wakufunzi wa ufuatiliaji juu ya ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatonayo na matumizi ya dawa.

Mafunzo hayo yalikuwa kwa watendaji wa afya kutoka Wilaya zote za mkoa wa Arusha.

Bw. Sillo amesema katika kudhibiti matumizi ya dawa zisizofaa TFDA imeondoa dawa ya sindano aina ya Kloramfeniko pamoja na aina nyingine za dawa hasa vidonge kwenye soko baada ya shirika la afya Duniani WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji.

No comments